Posts

Showing posts from March, 2024

JAMII IMEASWA KUTOA SADAKA KWA MOYO HATA KAMA KIDOGO.*

Image
Na Mwandishi wetu. Jamii imeaswa kutoa sadaka kwa moyo hata kama kidogo ili kila mmoja aweze kuishi katika mazingira mazuri hususani wakati huu wa mfungo wa Ramadhani. Hayo ameyasema jana Mwenyekiti wa Taasisi ya Ramadhan Charity Program 2024 Ahmed Misanga wakati taasisi yake ilipotoa sadaka katika kituo cha malezi cha Masjid Farouq Magorofani Wilayani Manyoni mkoani Singida.  Misanga amesema kuwa kutoa ni moyo hakuhitaji uwe na mali nyingi, na namna ya kuoneana huruma endapo mwenzako unamuona hana kitu basi unaweza kumsaidia. " Tunatoa sadaka kwa jamii pia naomba  jamii ifahamu kuwa kusaidia watu hakuhitaji uwe na mali nyingi bali moyo wako tu uwe unahitaji kusaidia pale unapomuona mwenzako hayupo katika wakati mzuri, leo hii Ramadhani Charity Program tupo hapa manyoni ili kusaida watu wenye uhitaji maalumu, " Misanga Katika hatua nyingne Misanga amewaomba jamii kuacha kuingia katika maadili mabaya kwani kuwa kwa sasa kumekuwa na  mmomonyoko wa maadili  amesema Qrua...