Posts

Showing posts from April, 2024

BILIONI 9.88 KUJENGA LAMI BARABARA YA DAREDA CENTRE- DAREDA MISSION.

Image
  Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amemuagiza Mtendaji Mkuu Wakala wa Barabara (TANROADS) kumsimamia Mkandarasi kampuni ya Jiangxi Geo Engineering kukamilisha kwa wakati ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Dareda hadi Dongobesh (km 60) sehemu ya kwanza ya Dareda Centre hadi Dareda Missioni (km 7) ili kuufungua kiuchumi Mkoa wa Manyara. Bashungwa amezungumza hayo Wilayani Babati Mkoani Manyara Aprili 06, 2024 wakati akishuhudia utiaji saini mkataba wa ujenzi wa barabara hiyo kati ya Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS) na kampuni ya M/s Jiangxi Geo Engineering (Group) Corporation ya China kwa gharama ya Shilingi Billioni 9.88.  “Tumempa Mkandarasi huyu kwa kuwa tayari anatekeleza miradi mingine ya barabara maeneo haya na jirani na tumemuongezea hii nyingine kwa kuwa si kilometa nyingi hivyo Mtendaji Mkuu sitaki kusikia visingizio nataka barabara hiyo ikamilike haraka maana hata Wakandarasi wa ndani kilometa saba wangeweza kuzijenga”, amesisitiza Bashungwa. ...

WAFADHILI WAMUUNGA MKONO RAIS SAMIA

Image
Serikali ya halmashauri ya Wilaya ya Babati imewataka wananchi kutunza miradi ya maendeleo ili iwe na tija kwenye jamii husika. Hayo yameelezwa na makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo,mh,Yahaya Loya wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji ktk shule ya msingi eluway kata ya nkaiti,kijiji cha Olasiti. Mradi huo uliojengwa na shirika la wine to water wenye thamani koya sh/million 61 umejengwa ktk shule ya msingi Olasiti ili kuwapunguzia adha wanafunzi wa shule hiyo kukatiza masomo na kufuata maji umbali mrefu Mh.Yahaya amewashukuru wafadhili hao kwa kujenga mradi huo wa maji utakaosaidia shule ya Olasiti na kijiji hicho kwa ujumla. Aidha amewaomba wananchi wa kijiji hicho kujitoa ktk uendelezaji na uendeshaji wa mradi huo. Vilevile amewapongeza wafadhili hao kwa kuunga juhudi za Rais DK.Samia Suluhu Hassan katika kuwasogezea wananchi huduma ya maji

MISANGA AENDELEA KUTOA MISAADA WILAYA YA MANYONI.

Image
  Na Mwandishi wetu. Taasisi ya Ramadhani Charity Program 2024 chini ya Mwenyekiti Mohamed Missanga imetoa msaada wa Box kilo 10  za tende kwa Sheikh wa walaya ya Manyoni kwajili ya wasaidizi wa ofisi ya Sheikh wa wilaya hiyo. Tasisi hiyo kwa kushirikina na Jamali Juma imewapatia msaada kina mama wajane mchele, Sukari, Mafuta, unga,  pamoja na pesa za mboga.  Missanga awataka wajane kuwa na umoja na kupendana ili watimize ndoto zao za kimaisha kwa kufanya kazi pamoja na biashara ndogondogo na kuwa karibu na Mungu. Taasisi hiyo inafanya harakati za kutoa misaada hii kila mwaka na mwaka huu tayari imetoa misaada kwa mikoa mitano na inaendelea kutoa hadi mwisho wa mwezi mtukufu.  "Tunaendelea kutoa misaada kadri tutakayojaaliwa," Misanga Mwisho.