WAFADHILI WAMUUNGA MKONO RAIS SAMIA
Serikali ya halmashauri ya Wilaya ya Babati imewataka wananchi kutunza miradi ya maendeleo ili iwe na tija kwenye jamii husika.
Hayo yameelezwa na makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo,mh,Yahaya Loya wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji ktk shule ya msingi eluway kata ya nkaiti,kijiji cha Olasiti.
Mradi huo uliojengwa na shirika la wine to water wenye thamani koya sh/million 61 umejengwa ktk shule ya msingi Olasiti ili kuwapunguzia adha wanafunzi wa shule hiyo kukatiza masomo na kufuata maji umbali mrefu
Mh.Yahaya amewashukuru wafadhili hao kwa kujenga mradi huo wa maji utakaosaidia shule ya Olasiti na kijiji hicho kwa ujumla.
Aidha amewaomba wananchi wa kijiji hicho kujitoa ktk uendelezaji na uendeshaji wa mradi huo.
Vilevile amewapongeza wafadhili hao kwa kuunga juhudi za Rais DK.Samia Suluhu Hassan katika kuwasogezea wananchi huduma ya maji

Comments
Post a Comment